Pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhandisi Marwa Lubilya katika kikao cha kujadili Utekelezaji,Mapendekezo na Hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali yaani (CAG -Controler and auditor General) kuishia June 2019/2020 katika Halmshauri ya Mji wa Makambako.
Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Makambako na kuhudhuriwa na wajumbe mbalimbali kutoka taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali ndani ya Halmashauri ya Mji wa Makambako na nje wa Mji wa Makambako.
Katika kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Njombe akiwa kama mgeni Rasmi amesisitiza kuwa pamoja na Halmashauri kupata hati safi mara nane(8) kutoka kwa (CAG) haimaanishi kuwa Halmashauri katika utekelezaji wake haina mapungufu kabisa hivyo ni vema kukaa na kujadili kwa pamoja namna ya kuzuia hoja za nyuma zisijirudie mara kwa mara na ikiwezekana kufuta hoja kabisa.
Aidha amepongeza ushirikiano uliopo kati ya CAG na Halmashauri na kuwa na imani ya kuweza kusaidia kufungwa kwa hoja na kwa wakati sahihi na weledi mkubwa ,Amegusia masuala ya ukusanyaji mapato kwa njia ya mfumo ili kuepuka suala la upotevu wa fedha mbichi kiholela ,Pia Suala zima la Mikopo ya vikundi vya Wanawake ,Vijana na watu wenye mahitaji maalumu ni vema sheria na kanuni zikafuatwa ili Mikopo hiyo irejeshwe kwa wakati ili na wengine wanufaike nayo kwa wakati muafaka.
Mkuu wa Mkoa pia amewakumbusha wajumbe husuani Madiwani,Watendaji kuendelea kuhimiza wananchi hasa wazazi kuchangia chakula kwa watoto mashuleni kwa wakati ili kuepusha adha ambazo zinaweza kuleta shida kwa wanafunzi pindi wanapokosa chakula kwa wakati, Sambamba na hilo ameongeza suala la Madawati ni vema pia utaratibu ukawekwa mapema ili kuepusha migogoro pale ambapo shule zinafunguliwa january suala la madawati na viti inakuwa shida si nzuri tushirikisne kutatua changamoto katika sekta hii ya elimu mapema.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa