Na. Lina Sanga
Katibu Tawala Mkoa wa Njombe, Bi. Judica Omari leo amefanya kikao kazi na timu ya menejimenti ya Halmashauri ya Mji Makambako,Watendaji wa Kata,Mitaa na Vijiji kuhusu ukusanyaji wa mapato,Kushughulikia na kutatua kero za wananchi uwajibikaji na kusikiliza changamoto zinazowakabili Watendaji na kupokea maoni yao.
Judica, amesisitiza uwajibikaji na uwazi katika utekelezaji wa majukumu ikiwa ni pamoja na utoaji wa risiti wananchi wanapolipia ushuru na mapato,ili kujenga imani kwa walipa kodi na kuongeza mapato ya Serikali.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa