Na. Lina Sanga
Rai hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Makambako, Mhe. Hanana Mfikwa katika kikao na Wenyeviti wa Mitaa na Vijiji,Watendaji wa Kata,Mitaa,Vijiji na timu ya menejimenti ya Halmashauri ya Mji Makambako ili kuwekana sawa katika baadhi ya masuala ya kiutendaji.
Mhe. Hanana amesema kuwa,kutokana na baadhi ya sintofahamu zilizoibuka chanzo kikuu ni kukosekana kwa mawasiliano baina ya Wenyeviti wa Mitaa na Vijiji na watendaji wa Mitaa na vijiji husika,hali iliyoibua maswali na hoja za kutoelewana katika utekelezaji wa majukumu ya kila mmoja.
Katika kikao hicho hoja mbalimbali ziliwasilishwa na Wenyeviti wa Mitaa na Vijiji ikiwa ni pamoja na kutopewa taarifa za utekelezaji wa masuala mbalimbali kutoka kwa Mkurugenzi,ikiwa ni pamoja na kutoitishwa kwa vikao kuhusu mabadiliko ya utekelezaji wa suala la ukusanyaji wa ushuru wa taka ambao awali Mitaa ilipewa jukumu hilo.
Ametoa agizo kwa watendaji wa mitaa na Vijiji kuhakikisha wanatekeleza wajibu wao,ikiwa ni pamoja na kufikisha taarifa ya masuala mbalimbali yanayofika mezani kwao,ili Wenyeviti waelewe nini kinafanyika kwenye Mitaa na Vijiji vyao na wao watekeleze wajibu wao kwa vyeo vyao.
Awali akijibu hoja hiyo,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Makambako, Ndg. Kenneth Haule amesema kuwa kila jambo ambalo linatekelezwa kwenye Kata,Mitaa na Vijiji ni lazima lipitie kwenye vikao vya kisheria na baada ya baraza la madiwani kubariki, ili kutoa nafasi kwa Madiwani na Watendaji wa Kata kushusha taarifa hizo ngazi ya Kata,Mitaa na Vijiji kwa taarifa na utekelezaji wa maagizo ya Mkutano wa baraza la Madiwani.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa