Na. Lina Sanga
Rai hiyo ilitolewa na Mhe. Deo Kasenyenda Sanga,Mbunge wa jimbo la Makambako katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani 2023, katika Halamshauri ya Mji Makambako,yaliyofanyika machi 7,2023 Mtaa wa soko la nyanya,Kata ya Mji Mwema.
Mhe. Sanga amesema kuwa ipo haja ya watu wote kuhakikisha wanashirikiana bega kwa bega na kina mama,katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo kuanzia ngazi ya familia hadi taifa,kwani wanawake wana uwezo wa kufanya mambo makubwa katika sekta mbalimbali wakiongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ameongeza kuwa,mama kuanzia ngazi ya familia ni jemedali mkuu na kiungo muhimu katika ustawi wa familia na jamii nzima,kwani hata katika masuala ya siasa kina mama wapo vizuri,wengi wameshika nafasi za uongozi na wanafanya mambo makubwa kwa ustawi wa taifa hili.
Aidha,ametoa wito kwa wananchi wote kuthamini watoto wote kwa kupinga ukatili na kushirikiana kuwalinda watoto dhidi ya ukatili ,kwa kutoa taarifa za vitendo vya ukatili ofisi za mitaa na Kituo cha polisi,kwa kutambua kuwa mtoto wa mwingine ni wa jamii yote ili kuwawezesha watoto kufikia ndoto zao.
Pia amesema kuwa,kwa kutambua umuhimu wa Kitengo cha dawati la jinsia ameunda kamati ya kusimamia ujenzi wa jengo la ofisi ya dawati la jinsia ,katika Kituo cha polisi Makambako ili kurahisisha watoto na wazazi kutoa taarifa za vitendo vya ukatili kwa urahisi.
Kamati hiyo inaundwa na wafanyabiashara wa Makambako ambao wanachangishana fedha kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo,Mwenyekiti ni Bw.Nurdin Mbilinyi maarufu kama NT Business,mtunza fedha wa kamati ni Bi. Benardetha Sanga maarufu kama Mama Chamanga.
Katika maadhimisho hayo Mhe. Sanga alizindua rasmi jukwaa la uchumi la wanawake katika Halmashauri ya Mji Makambako.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa