Mabadiliko ya baadhi ya mila katika jamii hasa zinamkandamiza mwanamke na kumpa mwanaume kipaumbele hususani katika suala la umiliki wa ardhi, yanahitajika ili kutoa nafasi sawa kwa wanawake na wanaume kumiliki na kutumia rasilimali kwa maendeleo,ustawi na uwezeshaji wanawake.
Kauli iyo ilitolewa jana na Mkuu wa Wilaya ya Makete, Mhe. Kissa Gwakisa Kasongwa katika Kilele cha maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani 2025, ambayo kwa Mkoa wa Njombe yamefanyika Kijiji cha Bulongwa,Halmashauri ya Makete.
Mhe. Kissa amewataka wanawake kujikita katika shughuli za kiuchumi ili kuepuka utegemezi wa kila kitu kutoka kwa wanaume,na kuwahimiza wanawake kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi badala ya kutegemea uteuzi wa viti maalum, kwani wana uwezo mkubwa wa kushiriki kikamilifu katika siasa na uongozi wa Nchi, hivyo wanapaswa kujiamini na kuchukua hatua za kuleta mabadiliko.
Mhe. Festo Sanga, Mbunge wa jimbo la Makete amewataka wanawake kuhakikisha wanalea watoto katika maadili mema ili kujenga kizazi bora,kwani mwanamke ana nafasi kubwa katika kuhakikisha watoto wanalelewa katika mazingira mazuri yanayowaandaa kuwa viongozi waadilifu na wazalendo wa Taifa.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Makete, Mhe. Christopher Fungo, amewapongeza wanawake kwa mshikamano ambao ni nguzo muhimu katika kuleta maendeleo na kuwataka waendelee kushirikiana na kuhamasishana ili kufanikisha malengo yao.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa