Na.Lina Sanga
Dar es salaam
Spika wa bunge la Tanzania,Mhe. Dkt. Tulia Ackson amewataka Maafisa habari wa Serikali kutofanya siri kwa taarifa ambazo sio za siri ili kuondoa upotoshaji kwa wananchi kwa kutoa habari sahihi kwa wakati na inapohitajika.
Dkt. Tulia ametoa wito huo leo katika kikao kazi cha 18 cha Maafisa habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali, kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam.
Amesema kuwa,ipo haja kwa Maafisa habari kufahamu taarifa zote za Halmashauri zao na Halmashauri zingine ,ili wananchi wanapohoji waweze kupata taarifa sahihi kwani Afisa habari anaaminiwa kuwa na taarifa sahihi.
"Afisa habari unatakiwa kufahamu taarifa mbalimbali zinazohusu Halmashauri yako lakini pia na Halmashauri zingine,ili mwananchi anapohoji kuhusu Halmashauri nyingine umsaidie kwa kumpa taarifa sahihi na kama huna majibu wasiliana na wahusika wa Halmashauri hiyo na umpe mwananchi taarifa sahihi anazozihitaji kuondoa upotoshaji",alisema Dkt. Tulia.
Ametoa rai kwa Maafisa habari kutilia maanani ilani ya Chama cha Mapinduzi kuhusu sekta ya habari na kuoanisha na majukumu ya sekta hiyo kwa ajili ya utekelezaji.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa