Mwezeshaji katika semina ya Saratani ya Mlango wa Kizazi akieleza wajumbe walioshiriki semina hiyo maana ya Saratani ya Mlango wa kizazi :Mlango wa kizazi (Cervix) ni kiungo katika tumbo la uzazi la Mwanamke.Saratani ya Mlango wa kizazi inasababishwa na virusi vijulikananvyo kitaalamu kama Human Papiloma Virus (HPV) ,
.Ni ugonjwa hatari na unaoua wanawake wengi nchi zinazoendelea ,
.HPV huambukizwa kwa njia ya Ngono toka kwa mtu mwenye virusi hivyo wakati virusi hivyo pia huambukiza koo au sehemu ya haja kubwa kwa jamii zinazofanya Ngono kinyume na maumbile.
.Maambukizi yameenea sana ulimwenguni Kila mtu akikanza kushiriki ngono anakuwa katika hatari ya kupata maambukizi hayo ya HPV.
.Tafiti zinaonesha kuwa katika kila wanawake wanne wanaoshiriki ngono watatu wanapata maambukizi ya HPV wakati fulani katika maisha yao.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa