MAKAMBAKO KINARA UFUNGAJI WA HESABU ZA MWISHO TANZANIA BARA KUNDI LA HALMASHAURI ZIPATAZO 185
Halmashauri ya mji wa Makambako imeibuka kinara katika ufungaji wa hesabu za mwisho Tanzania miongoni mwa Halmashauri
zipatazo 185 za Tanzania bara. Ushindi huo ulitangazwa kataka hafla iliyo andaliwa na bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi
yaani NBAA mnamo tarehe 07/12/2019 Bunju Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtandaji wa NBAA CPA Pius Maneno akikabidhi zawadi kwa Mkuu wa Idara ya Fedha H/Mji Makambako Bw.Robert Sinnah
Akizungumzia ushindi huo mkuu wa idara ya Fedha na Biashara katika Halmashauri ya Mji waMakambako Bw. Robert Sinnah alisema
Ushindi huo ni ishara tosha ya ufanyaji kazi kwa bidii,ueledi na ushirikiano unaoneshwa na idara iliyo chini yake licha ya kwamba
Halmashauri ya Mji wa Makambako bado ni changa mno(ilianzishwa mwaka 2012).
Pia amepongeza kitengo kizima cha ufungaji wa hesabu za mwisho kikiongozwa na CPA Suphian Juma kwa kazi nzuri waliofanya.
Aidha, mkuu wa kitengo cha Ukaguzi wa ndani CPA Amen-Rabi Isack amesema licha ya ushindi huo kitengo chake hakitobweteka na
kuahidi kuendelea kuchapa kazi kwa nguvu zaidi ili kuendelea kudhibiti pesa za serikali.
Waliokaa kutoka kulia: CPA Amen-Rabi Isaack,Bw.Robert Sinnah Waliosimama Kutoka kushoto:CPA Suphian Juma,CPA Okoa Fungo,
CPA Baraka Manyangu
Wahasibu walioshiriki katika ufungaji mahesabu kwa mwaka 2019 ni
1.CPA Suphian Juma
2.CPA Okoa Fungo
3.Bw.Andrea Mtewa
4.Bi.Adela Mgaya
5.Bw.Priscus Mushi
Wakaguzi wa Ndani
CPA Amen-Rabi Isack
CPA Baraka Manyangu.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa