Na. Lina Sanga
Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Dkt Philip Mpango ameitaka TRA Migoli na Iringa kuhakikisha changamoto ya ucheleweshaji wa shehena za parachichi zinazosafirishwa inaondolewa.
Mhe. Mpango ametoa agizo hilo leo mara baada ya kupokea changamoto anazokabiliana nazo mwekezaji wa kiwanda cha usindikaji wa parachichi AVOAFRICA,kilichopo Mtaa wa Majengo, katika Halmashauri ya Mji Makambako.
Amesema kuwa,kitendo cha TRA Migoli na Iringa kuzuia shehena ya parachichi kwa muda mrefu,inaweza kumsababishia mwekezaji hasara kubwa kwani zao hilo ni mali mbichi ambayo inaweza kuharibika kiurahisi.
Aidha, ametoa wito kwa wananchi wote nchini katika maeneo yanayolimwa zao la parachichi kutambua kilimo hicho ni fursa na kuwataka kuitumia fursa hiyo vizuri ,kwani soko la zao hilo ni kubwa na Serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya usafirishaji na kwa sasa ndege ya mizigo imenunuliwa ili kuwezesha wawekezaji kusafirisha mizigo ikiwa ni pamoja na parachichi.
Pia,amesema kuwa changamoto ya uwanja wa ndege wa Mkoa wa Njombe ameisikia na kuahidi kuishughulikia kwani Serikali ya Mama Samia ipo kazini ikiwa na lengo la kuhakikisha maisha bora kwa watanzania.
Amepongeza uwepo wa kiwanda cha AVOAFRICA ambacho uwekezaji wakeumegharimu dola za kimarekani takribani mil. 4.8 na kueleza kuwa kiwanda hicho ni cha mfano na kuwataka waandishi wa habari kueneza uwepo wa kiwanda hicho ili vijana wengi wavutiwe kuwekeza katika kilimo cha parachichi.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa