Mkuu wa wilaya ya Njombe Bi Ruthi Msafiri akizungumza kama Mgeni Rasmi Katika Semina ya Saratani ya Mlango wa kizazi iliyoandaliwa na shirika la JPHEGO kwa kushirikiana na wataalamu wa afya Wilaya ya Njombe kwa Halmashauri tatu (3) yakuwa wajumbe waliohudhuria semina hiyo wasikilize kwa umakini mkubwa na wawe mabalozi katika jamii juu ya saratani ya Mlango wa kizazi kwa ngazi ya familia mpaka Taifa.Aidha Mikakati na Maazimio ya Semina hiyo yafanyiwe kazi kwa Halmashauri zote tatu zilizo hudhuria semina hiyo ( Makambako ,Njombe TC ,na Njombe DC hasa chanjo ya kuzuia Saratani ya Mlango wa kizazi kwa mabinti wa miaka kumi nanne (14), ili waje kuwa akinamama wenye afya bora hapo baadae walioepuka Saratani ya Mlango wa kizazi kwa Wanawake kwa kukingwa na chanjo hiyo mapema.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa