Na. Lina Sanga
Mbeya
Katika picha ni baadhi ya wakulima na wafugaji kutoka Halmashauri ya Mji Makambako wakitoa elimu kwa wananchi waliotembelea banda la Halmashauri Ya Mji Makambako katika Maonyesho ya nanenane 2022,katika viwanja vya John Mwakangale Mkoani Mbeya.
Katika banda la Halmashauri ya Mji Makambako kuna miradi mbalimbali ya Ufugaji kama unenepeshaji Ng'ombe na Mfugaji anakaribishwa kujifunza namna ya uandaaji wa chakula cha ng'ombe ili aweze kuuza nyama kimataifa.
Pia kuna ufugaji wa kuku na utotoleshaji wa vifaranga unaomuwezesha mfugaji kufuga kuku na kutotolesha vifaranga kwa kutumia mashine zinazotumia mafuta ya taa na kujipatia kipato.
Lakini pia ufugaji wa samaki aina ya sato na kambale ambapo mfugaji anaweza anzisha mradi huu kwa gharama ndogo kwa kutengeneza mabwawa mazuri yanayogharimu fedha kidogo.
Aidha,katika banda la Halmashauri ya Mji Makambako kuna wataalamu wa kilimo na kifugo lakini pia wakulima na washauri wa masuala ya kilimo na mifugo na namna bora ya utunzaji wa mazingira wakati wa utekelezaji wa shughuli za kilimo.
Pia kuna zana mbalimbali za kilimo zinazomuwezesha mkulima kulima kilimo cha kisasa kwa muda mfupi na kupata mazao.
Wananchi wote mnakaribishwa katika banda la Halmashauri ya Mji Makambako kujifunza mbinu mbalimbali za kilimo na mifugo pamoja na ujasiriamali,lakini pia kununua bidhaa mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya nyumbani kama unga,kuku,maziwa,mvinyo wa nyanya,viungo vya chakula na kujifunza masuala yanayohusu vyama vya ushirika.
Kauli mbiu ya maonyesho ya nanenane kwa mwaka huu"Agenda 10/30 Kilimo ni Biashara,Shiriki kuhesabiwa kwa mipango bora ya kilimo,Mifugo na Uvuvi".
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa