Na. Lina Sanga
Iringa
Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar,Mhe. Othman Masoud othman amelitaka shirika la ndege la Air Tanzania (ATCL) kuendelea kuimarisha safari za ndege katika Mikoa ya kusini, yenye hazina kubwa ya vivutio vya utalii ili kuchochea ukuaji wa shughuli za utalii na kuchangia maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
Mhe. Othman ametoa rai hiyo leo alipokuwa akihutubia wadau wa utalii na wananchi waliofika katika viwanja vya maonyesho ya Utalii karibu kusini 2022 ,Kihesa Kilolo mkoani Iringa ambapo maonyesho hayo yamehitimishwa leo.
Kabla ya kufunga rasmi maonyesho hayo kwa mwaka huu Mhe. Othman amesema ipo haja ya mikoa ya kusini kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii kauibua mazao Mapya ya utalii,na kuyatangaza ili kuwavutia Watalii kwa kuzingatia mpango wa Taifa wa tatu wa maendeleo wa miaka Mitano kuanzia mwaka 2021/2022 hadi 2025/2026.
Aidha, ametoa wito kwa mikoa yote nchini kuhakikisha inaajiri Maafisa Utalii pamoja na kuunda kamati za ushauri za utalii kwa ngazi ya Mkoa,ambazo zitahusisha wadau mbalimbali kutoka katika mikoa husika.
Pia, amezitaka Mamlaka za Serikali za Mitaa kutenga maeneo ya uwekezaji na kuweka miundombinu muhimu ya kuvutia uwekezaji wa shughuli za utalii,pamoja na kuendeleza utalii wa fukwe na mazao mengine ya utalii yenye fursa kwa ufanisi mkubwa.
Ametoa wito kwa Mikoa yote ya kusini kuanza maandalizi na uratibu wa maonyesho hayo kwa mwaka 2023 mapema, ili kuvutia waoneshaji wengi zaidi pamoja na wanunuzi wa bidhaa za utalii wa Kimataifa.
Maonyesho ya Utali karibu kusini kwa mwaka 2023 yanatarajiwa kufanyika septemba 23.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa