Halmashauri ya Mji wa Makambako imepokea mashine 43 (arobaini na tatu ) za kukusanyia mapato kutoka serikali kuu kupitia wizara ya TAMISEMI. Hafla ya kupokea mashine hizo ambazo zimetolewa msaada kutoka Norway ilifanyika tarehe 22/01/2020 katika Jengo la LAPF Dodoma.
Halmashauri imezipokea na kuziandaa na ziko tayari kwa matumizi.
Akizungumza baada ya kukabidhi mashine hizo kwa Kitengo cha TEHAMA Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Makambako Ndg.Paulo Sostheness Malala ametoa rai kwa watumishi wa halmashauri na wadau kwa ujumla kutunza mashine hizo na kuchapa kazi kwa bidi ili kufikia na kuvuka malengo ya makusanyo ya mapato.
Hata hivyo uwepo wa mashine hizi mpya haitamaananisha kusitishwa kwa mashine za awali, Halmashauri kupitia kitengo cha TEHAMA itasimamia uhuishwaji wa mashine za awali na program mpya ili kuwezesha kufikia malengo ya ukusanyaji wa mapato kwa ufanisi.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa