Katika picha ni matukio ya Mbio maalum za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2021 katika Wilaya ya Njombe Ambapo Mbio hizo maalum za Mwenge wa Uhuru zimebebwa na kauli mbiu kuu ya "Tehama ni Msingi wa Taifa endelevu itumike kwa usahihi na uwajibikaji."
Wakati kauli ndogondogo ni pamoja na:Kupambana na Rushwa ni jukumu langu,Mshikamano wa Kitaifa tuwajibike kwa pamoja ,Tujenge Jamii yenye Afya imara kwa kuzingatia lishe bora,Zero Malaria inaanza na mimi nachukua hatua kuitokomeza ,Elimu sahihi ya Dawa za kulevya huboresha huduma kwa waraibu;chukua hatua.
Katika msafara wa mbio maalumu za Mwenge wa Uhuru Mwaka huu umeongozwa na kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa LUTEN KANAL Josephine Paul Mwambashi akiambatana na LUTEN KANAL Ramadhani Ally Mshamu,Coplo Rehema Ally Haji ,LUTEN KANAL Geofrey Juma Aroni ,LUTEN KANAL Musa Hassan Musa na PTE Dismas Egno Mvula.
Akitoa salaamu za Mbio maalumu za Mwenge wa Uhuru LUTEN JOSEPHINE PAULO MWAMBASHI mara baada ya kuhitimisha zoezi la kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo amesema kuwa watu wanaotumia madawa ya kulevya hawatakiwi kunyanyapaliwa bali wapewe elimu ili watambue athari za kutumia madawa hayo na waachane nayo kwani yanadumaza utendaji kazi na nguvu kazi ya taifa jambo ambalo linaweza kuleta madhara makubwa katika taifa letu.
Mwambashi ameongeza kuwa kutokana na vijana wengi kujihusisha na madawa ya kulevya kumesababisha madhara makubwa kwani wahanga wamelifanya taifa likose nguvu kazi kutokana na wengi wao kukumbwa na magonjwa mbalimbali kama vile maambukizi makubwa ya VVU jambo ambalo taifa litapoteza nguvu kazi kubwa na katika janga la Rushwa amesema jamii ikatae Rushwa kwakuwa Rushwa ni adui wa haki na watu wengi wanapoteza haki zao za msingi kwa sababu ya Rushwa hivyo kuikataa Rushwa ni jukumu letu sote.
Awali akipokea Mbio maalum za Mwenge wa Uhuru kutoka Wilaya ya Ludewa Mkuu wa Wilaya ya Njombe KISSA GWAKISA KASONGWA amesema kuwa Mwenge wa Uhuru utazindua jumla ya miradi ya kimaendeleo kumi na moja (11) ya serikali na isiyo ya kiserikali yenye thamani zaidi ya shilingi Billion mbili.
Mwenge huo wa uhuru umehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Makada mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi(CCM) ,Wakurugenzi wa Halmashauri zote za wilaya ya Njombe ,Wakuu wa idara na vitengo pamoja na wananchi wa sehemu mbalimbali zenye miradi ambayo imepitiwa na Mbio maalumu za Mwenge wa Uhuru mwaka huu.Kazi Iendelee.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa