Pichani aliyesimama kama mzungumzaji ni Mbunge wa Jimbo la Makambako Ndg Deo Sanga katika kikao cha Kujadili Rasimu ya Mpango wa Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 na Mapitio ya Mwaka 2019/2020 na nusu 2020/2021 zoezi ambalo limenda sambamba na uzinduzi wa gari la kubeba taka katika Halmashaur ya Mji wa Makambako ,akichangia katika mchanganuo wa Bajeti hiyo hasa katika suala la Wananchi kulipwa fidia ambapo amagusia eneo la Mtaa wa Polisi kuwa Wananchi wanaishi katika Mazingira Magumu kama vyoo vyao vimebomoka hawaruhusiwi kufanya ukarabati wowote unao husiana na ujenzi hivo ameziomba mamalaka husika kulitizama hilo mbali na kuwa tayari kama Mbunge wa jimbo la Makambako ameshakutana na Waziri wa Mambo ya Ndani na kuzungumza nae suala hilo la fidia kwa wananachi hao,
Ameomba pia Watumishi kujitoa katika masuala mazama ya kuhudhuria vikao mbalimbli kwani vikao hutatua kero ,Vikao hujenga hoja hivyo basi hakuna budi kuwatuma wawakilishi katika vikao mbalimbali kama hakuna ulazima ,Waje wasimamaizi wakuu wa Taasisi husika , Hii ni mara baada ya utambulisho wa taasisi mbalimbali za kiserikali na zisizo za kiresikali kutuma wawakilishi wao baaada ya kuja wao kama wasimamizi wakuu wa taasisi hizo 'Nimeona wakati wa utambulisho hapa wengi wanasema na muwakilisha fulani kwanini wasije wao' ? kuna nini alisema Sanga hii sio nzuri kuna maswali mengine wawakilishi mtashindwa kujibu lakini wakija wakuu wenu itakuwa rahisi kuyajibu.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa