Na. Lina Sanga
Njombe
Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Tawala Mkoa wa Njombe,Bi. Judica Omari katika kilele cha maadhimisho ya miaka 61 ya uhuru wa Tanzania Bara katika Wilaya ya Njombe,yaliyofanyika katika ukumbi wa Njombe Sekondari.
Bi. Judica amebainisha kuwa,katika miaka 61 ya uhuru maisha ya wananchi wa Mkoa wa Njombe yamezidi kuimarika siku hadi siku,kwa kuishi katika nyumba bora na kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi na kuongeza kasi ya ukuaji wa pato la Mkoa kutoka Mil. 5.69 Njombe ilivyokuwa Wilaya chini ya Mkoa wa Iringa hadi kufikia trillion 3.2 kwa mwaka na pato la kila mwananchi kupanda kutoka shilingi 103 Njombe ilivyokuwa Wilaya na kufikia Mil. 3.8 kwa mwaka baada ya kupandishwa hadhi na kuwa Mkoa mwaka 2012.
Amesema kuwa kwa upande wa sekta ya elimu,tangu mwaka 1961 Njombe ilikuwa na jumla ya shule za msingi 90 na sekondari 6,shule 3 za Serikali na 3 za watu binafsi na hadi kufikia mwaka huu 2022,Mkoa wa Njombe una jumla ya shule za msingi 544 na shule za sekondari 139,ambapo shule 99 zinamilikiwa na Serikali na shule 40 ni shule binafsi hali inayochangia ukuaji wa sekta ya elimu kwani kila mwanafunzi anapata nafasi ya kujiunga na shule bila ubaguzi kama ilivyokuwa miaka ya ukoloni.
Katika sekta ya afya,Mwaka 1961 Njombe ilikuwa na Zahanati 22 na Hospitali 3 na hakukuwa na vituo vya afya kabisa,tofauti na sasa ambapo kuna jumla ya vituo vya kutolea huduma za Afya 337,Hospitali 22,Vituo vya afya 44 ngazi ya Kata na Zahanati 271 kwa mujibu wa Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.
Aidha katika sekta ya barabara, Bi. Judica amebainisha kuwa mwaka 1961 Njombe haikuwa na barabara ya lami na mtandao wa barabara ulikuwa na urefu wa 1,209KM kati ya hizo 76KM zilikuwa barabara za vumbi na 1,133KM kiwango cha changarawe na Udogo, kwa sasa mabadiliko makubwa yametokea ambapo Wakala wa barabara nchini (TANROADS) hadi mwaka huu anahudumia matengenezo ya barabara zenye jumla ya urefu wa 1,188KM kati ya hizo 251KM zina kiwango cha lami na 937KM zina kiwango cha chanagarawe na udongo.
Ameongeza kuwa Mkoa wa Njombe una mtandao wa barabara wenye urefu wa 5,208KM zinazohudumiwa na Wakala wa barabara vijijini na Mijini (TARURA) ,ambapo jumla ya 42KM zina kiwango cha lami, 1,293KM kiwango cha changarawe na 3,873KM zenye kiwango cha udongo.
Kwa upande wa sekta ya maji katika Mkoa wa Njombe amesema kuwa ,huduma ya maji safi na salama Inapatikana kwa asilimia 73 maeneo ya Mijini na asilimia 83 katika maeneo ya vijijini na jitihada mbalimbali zinaendelea kufanyika ili huduma ya maji ifikie asilimia za kitaifa.
Upande wa nishati,imeelezwa kuwa kati ya Vijiji 381 vya Mkoa wa Njombe Vijiji 298 vina huduma ya umeme na Vijiji 83 vinaendelea kuunganishiwa huduma ya umeme chini ya mradi wa REA III mzunguko wa pili, ambao ulizinduliwa mwezi septemba,2021 na mwishoni mwa mwaka huu wa fedha 2022/2023 Serikali inategemea Vijiji vyote vya Mkoa wa Njombe kupata huduma ya umeme na kuanza mradi mpya wa kufanya ujazilizo wa umeme ngazi ya Vitongoji ambapo kwa sasa huduma ya umeme katika ngazi ya Vitongoji ni asilimia 50.
Mkoa wa Njombe una jumla ya wilaya 4,Halmashauri 6,tarafa 18,Kata 107,Mitaa 82,Vijiji 381,Vitongoji 1,839 ambapo Halmashauri ya Mji Makambako ina Kata 12,Mitaa 54,Vijiji 14,Vitongoji 67,Shule za sekondari 15,binafsi 5 na shule za Serikali 10 na shule za Msingi 51,shule za Serikali 45 na binafsi 6 barabara za mitaa za kiwango cha lami kilomita 12,Vituo vya kutolea huduma za afya vya Serikali 3,Zahanati 7 na Hospitali 1.
"Amani na Umoja ni Nguzo ya Maendeleo Yetu"
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa