Na. Lina Sanga
Halmashauri ya Mji Makambako kupitia Mfuko wa maendeleo ya jamii –TASAF kwa mwaka wa fedha 2021/2022 ilipokea zaidi ya Mil.73 za miradi ya kupunguza Umasikini (OPEC IV) inayofadhiliwa na TASAF awamu ya tatu.kwa ajili ya ufunguzi na ukarabati wa barabara zenye urefu wa kilomita 4.22 katika Kijiji cha Ibatu na Kitandililo.
Agnes Kihungu,msimamizi wa mradi wa ufunguzi wa barabara kijiji cha Ibatu amesema kuwa, kukamilika kwa mradi wa ufunguzi wa barabara hiyo inayounganisha vitongoji viwili,Kitongoji cha Isaula na Kitongoji cha Ilengititu itasaidia Kijiji kukua kwa kasi,watu watajenga nyumba na huduma za kijamii zitasogea ikiwa ni pamoja na usafiri wa magari ya mizigo na abiria.
Barabara kijiji cha Ibatu inayofunguliwa na kuunganisha Vitongoji viwili,Kitongoji cha Isaula na Kitongoji cha Ilengititu.
Ametoa shukurani kwa Serikali na TASAF kwa kutoa fedha kwa ajili ya ufunguzi na ukarabati wa barabara,fedha za walengwa wa TASAF na kutoa ajira za muda kwa wananchi wa maeneo ambayo miradi inatekelezwa na kuongeza pato la Kijiji na mwananchi mmoja mmoja.
Aidha,amebainisha kuwa kupitia mradi huo wa barabara jumla ya watu 54 wanufaika wa TASAF katika kijiji cha Ibatu, wamepata ajira ya muda ya miezi mitatu na kuongeza pato la kaya zao.
Naye, Eliezel Mlawa (55) mmoja wa wanufaika wa TASAF wanaofanya kazi katika mradi wa ufunguzi wa barabara Kijiji cha Ibatu,amesema kupitia TASAF amepata fedha zilizomuwezesha kusomesha watoto,matumizi ya familia na ujenzi wa nyumba ,na kumpa ajira ya muda ambayo anapata fedha kwa ajili ya kuongeza kipato cha kaya yake.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa