Na. Lina Sanga
Ili kukamilisha mpango wa Serikali wa kila Kata kuwa na Kituo cha afya na Mtaa au Kijiji kuwa na Zahanati, Halmashauri ya Mji Makambako kupitia Mfuko wa maendeleo ya jamii –TASAF kwa mwaka wa fedha 2019/2020, imefanikiwa kujenga Zahanati ya Kitisi iliyopo Mtaa wa Lupila katika Kata ya Kitisi ili kusogeza huduma kwa jamii.
Bi. Grace Ngole,Kaimu Msimamizi wa Zahanati ya Kitisi amesema kuwa katika Zahanati hiyo huduma mbalimbali za afya zinatolewa kwa masaa 12 ikiwa ni pamoja na huduma za kliniki kwa wajawazito na watoto,huduma za chanjo,uzazi wa mpango,matibabu kwa wagonjwa wan je na huduma endelevu za kufubaza makali ya UKIMWI.
Amesema kuwa, Zahanati hiyo ilianza kutumika rasmi mnamo agosti 2020 na kwa sasa wanahudumia hadi wagonjwa 50 kwa siku , wamama wajawazito hadi 30 na kliniki ya watoto 60 kwa siku ya ijumaa ambayo hutolewa chanjo na siku za kawaida watoto 50.
Jengo la Zahanati ya Kitisi.
“Siku za mwanzo tulikuwa na wagonjwa wachache sana waliofika kupata huduma,nadhani ni kutokana na kukosekana kwa taarifa za huduma zinazopatikana katika Zahanati hii,watu walishazoea kupata huduma Kituo cha Afya Makambako lakini sasa wakazi wote wa Kata ya Kitisi ni lazima aanzie hapa kupata huduma na endapo kuna sababu maalumu atapewa ruhusa kwenda Kituo cha afya”,alisema Bi. Ngole.
Ametoa wito kwa wananchi wote kufika katika Zahanati hiyo kupata huduma za afya kwani Serikali kupitia Mfuko wa maendeleo ya jamii –TASAF, inawajari wananchi kwa kuwasogezea huduma zote muhimu ikiwa ni pamoja na vituo vya kutolea huduma za afya.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa