Pichani ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Makambako Paulo Malala,akizungumza na wajumbe wakati wa uzinduzi wa kamati ya MipangoMiji Halmashauri ya Mji wa Makambako zoezi ambalo lilienda sambamba na Uchaguzi wa Viongozi wa kamati hiyo yaani Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa kamati lengo likiwa ni kushirikiana kwa pamoja katika kutatua na kuzuia migogoro ya Ardhi katika Halmashauri ya Mji wa Makambako.
Wakati wa uzinduzi wa kamati hiyo Malala amewasisitiza wajumbe kufanya kazi kwa weledi mkubwa kwa kutumia taaluma zao kutokana na wajumbe kuwatayari na taaluma husika za masuala ya Ardhi Mfano:Idara ya Mazingira ,Tarura na Ardhi wenyewe idara hizi zikishirikina kwa pamoja zinaweza kuleta matokeo chanya ,katika kusaidia jamii ya Makambako hususani katika masuala mazima ya Ardhi.
"Fuateni sheria na kanuni zilizowekwa na Mamlaka husika ili kuondoa migogoro ,ugomvi na uhasama unaoweza kujitokeza kama msipofuata sheria za mamlaka husika ,Muda mwingine jitoeni sadaka kwaajili ya Wananchi,wapeni msaada ili wasijekutamka kuwa mna maslahi binafsi kwenye sekta ya Ardhi" ,Paulo Malala.
Ameyazungumza hayo mara baada ya uchaguzi wa viongozi wa uainishaji kazi za MipangoMiji katika mamlaka za upangaji Miji Nchini ambapo katika uchaguzi huo nafasi ya Mwenyekiti yalipendekezwa majina mawili ambayo ni APPIA MAYEMBA (Mkuu wa idara ya Mazangira Halmashauri ya Mji wa Makambako) na ELIUDI MWAKIBOMBAKI (Mkuu wa idara ya Mipango Halmashauri ya Maji wa Makambako ) wajumbe kumi (10) walipiga kura kumuchagua Mwenyekiti ambapo APPIA MAYEMBA Aliibuka mshindi kwa kura sita dhidi ya ELIUD MWAKIBOMBAKI ambaye alipata kura nne( 4) hivyo kufanya APPIA kuwa Mwenyekiti wa kamati .
Wakati huo nafasi ya Makamu Mwenyekiti yalipendekezwa majina mawili ambayo ni CLAUDIA KIPAPI(Afisa Ardhi) NA ELIUD MWAKIBOMBAKI na wajumbe walipiga kura kumchagua Makamu Mwenyekiti ambapo ELIUDI MWAKIBOMBAKI aliibuka mshindi kwa kura sita dhidi ya CLAUDIA KIPAPI aliyepata kura nne(4).
Mara baada ya Uchaguzi na uzinduzi wa kamati ya MipangoMiji kikao cha kamati kikajadili maombi ya kubadilisha matumizi ya Ardhi takribani kwa viwanja nane(8) zoezi ambalo lilisimamiwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Appia Mayemba ,Wajumbe walijadili na kukubali kubadii matumizi ya viwanja hivyo lakini wakapendekeza kuwa kikao cha kamati ijayo ni vema wakatembele kwanza maeneo husika kabla ya kuanza kujadili zoezi zima la kubadilisha matumiza ya viwanja hivo ,Kwakuwa Majukumu ya kamati hiyo ni pamoja na kukagua na kupitisha Mipango ya jumla ya kina inayokidhi vigezo kwaajili ya kuainishwa na ofisi ya Ardhi Mkoa na kutoa mapendekezo yenye tija wakati wote, Kushauri juu ya maeneo muhimu katika mamulaka za upangaji ,kukagua na kupitisha maombi na mabadiliko ya matumizi ya Ardhi na kukagua maeneo yanayotiliwa shaka .
Akifunga kikao cha kamati hiyo Mwenyekiti Appia amewasisitiza wajumbe na kuwaomba kuzingatia wito uliotolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Makambako kuwa viongozi na wajumbe wafanye kazi kwa weledi mkubwa kwa lengo la kuepusha migogoro isiyo na ulazima katika Mji wa Makambako."Ndg wajumbe Mkurugenzi katoa wito mzuri tuufuate kwaajili ya maslahi ya Wananchi kwa ujumla Amesema APPIA"."
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa