Na. Lina Sanga
Hayo yameelezwa na Flaviana Mamkwe, Msimamizi wa sekta ya ardhi katika mkutano wa uhamasishaji wa zoezi la urasimishaji katika Mtaa wa Mashujaa na Kisiwani,katika Kata ya Kivavi.
Mamkwe amesema kuwa,urasimishaji ni muhimu ili kila mwananchi aweze kumilikishwa ardhi , ili hati ya kiwanja itumike kwa manufaa kama dhamana katika masuala ya kisheria na kiuchumi, hivyo kwa maeneo yote ambayo yatarasimishwa leseni za makazi hazitatumika tena kama dhamana bali ni hati pekee.
Kenneth Haule, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Makambako amewataka wananchi kuitumia fursa hiyo ya kulipia 130,000 kwa ajili ya urasimishaji kwa kila kiwanja, kwani hiyo ni ofa kama ilivyokuwa ofa ya kuunganishiwa umeme kwa 27,000.
Naye, Mzee Jobu Kaduma, mkazi wa Mtaa wa Mashujaa amewataka wananchi kuitikia zoezi la urasimishaji,ili Mtaa upangike vizuri na kutenga maeneo ya huduma za kijamii kama shule na vituo vya Afya.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa