Na. Lina Sanga
Miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji kujengwa katika mikoa ya Nyanda za juu kusini ili kuwawezesha wakulima katika mikoa hiyo kulima mwaka mzima,baada ya tathimini ya ujenzi wa miundombinu hiyo kukamilika.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Kilimo,Mhe. Hussein Bashe alipokuwa akitoa salamu kwa wakazi wa Halmashauri ya Mji Makambako leo,waliofika kumsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Mhe. Bashe amesema kuwa Mikoa ya nyanda za juu kusini ikiwa ni pamoja na Mkoa wa Njombe,ni mikoa yenye rasilimali kubwa ya maji lakini muelekeo wa Serikali katika ujenzi wa miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji ni kuanzia Mkoa wa Morogoro ,Iringa, Njombe, Mbeya, Ruvuma, Songwe, Rukwa na Katavi.
Amesema kuwa,Mikoa hiyo itapewa kipaumbele katika ujenzi wa miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji,ili kuwawezesha wakulima kulima mwaka mzima kutokana na Mikoa hiyo kuzalisha chakula kwa wingi nchini.
Ametoa wito kwa wakulima wote nchini kujisajili kwa ajili ya kupata mbolea za ruzuku,na kuanzia agosti 15 waanze kuandaa mashamba kwa ajili ya kuanza shughuli za kilimo,lakini pia kutoa taarifa wanapobaini udanganyifu wa uuzaji wa mbolea ya ruzuku ili waendelee kunufaika na ruzuku hiyo.
Mwisho amewataka wakulima kuhakikisha wanabakisha akiba ya chakula kwa ajili ya familia,kwani Serikali imefungua mipaka ya kuuza mazao na haimzuii mkulima kuuza mazao yake.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa