Na. Lina Sanga
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Makambako, Kenneth Haule jana amewatembelea wahanga wa mvua na upepo mkali Katika Mtaa wa Mludza,Mkolango,Itipingi na Mgewalala katika Kata ya Mlowa ambao nyumba zao zilipata madhara ya kuezuliwa paa na nyingine kubomoka kuta mnamo Novemba 29,2024 kuanzia majira ya saa tisa alasiri.
Haule akiongozana na baadhi ya wajumbe wa kamati ya maafa ngazi ya Halmashauri ambayo ilishafika kwa waathirika hao na kukusanya takwimu kwa ajili ya kufanya tathmini, amewapa pole wahanga hao na kuwataka kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki cha mpito wakati taratibu zingine zikiendelea kufanyika.
Aidha, amewashukuru wananchi wa Mitaa hiyo,wadau na Mhe. Odillo Fute ambaye ndiye diwani wa Kata hiyo kwa kuchukua hatua za haraka za kufanya marekebisho kwa wahanga wasiopungua watano kati ya 13 kupitia michango mbalimbali ikiwa ni pamoja na fedha taslimu na kuajiri mafundi.
Pia, ametoa ushauri kwa Wenyeviti wa Mitaa hiyo na viongozi wote kwa ujumla kutoa ushauri kwa wananchi wa kufuata taratibu za ujenzi wa nyumba, ikiwa ni pamoja na kujenga msingi imara wa nyumba pamoja na lenta ili nyumba iwe imara zaidi.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa