Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Makambako Paulo S Malala akizungumza na Wafanyakazi na Watendaji wa Halmashauri ya Mji wa Makambako katika kikao kilochofanyika mnamo tarehe 31 March katika Halmashauri ya Mji wa Makambako kikao ambacho Mwenyekiti wa kikao hicho akiwa ni Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi Ruth Msafiri ,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Makambako amegusia suala la usafi kwa WafanyakazI na Watendaji .
Mbali na kuwa Mkuu wa kikao hicho ambae ni Mkuu wa Wilaya Ya Njombe kugusia suala la weledi kazini na kuwa na mpango kazi kwa wafanyakazi na watendaji kuwa na tabia ya kuwa na Ratiba za kuwaongoza nini cha kufanya kuanzia mtu akiwa hajotoka nyumbani kwake ajue cha kufanya huko kazini ''kuna watu mtu anaenda kazini hajui hata nini anaenda kufanya hukokazini ni aibu kwa mtu anayetambua maana ya uwajibikaji ''Mkuu wa Wilaya ya Njombe''. Ameongoza pia masula ya kujitoa katika masuala mazima ya kuleta maendeleo katika taifa letu ya kuwa tuache kuwaamini watu kutoka nje kuwa wao ndo wenye kuleta maendelo ya Taifa la Tanzania HAPANA jukumu la maendeleo ya Tanzania ni kwa Watanzania ,Puuzeni maneno yenye kutugawa Yenye kuleta chuki kati yetu ,acheni matumizi mabaya ya mitandao na kuunga mkono vitu ambavyo havina msingi hasa kwenye mitandao ya kijamii na simameni kwaajili ya maendelo ya Tanzania haijalishi tupo katika maombolezo kazi inaendelea na tumuunge mkono Raisi wetu wa sasa Mama Samiah Suluhu Hassan kwa kuyaendeleza yaliyoachwa Hayati Magufuli kwa Taifa letu.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Makambako nae amegusia suala la usafi katika Mji wa Makambako kuwa hataki taka kuzagaa ovyo katika Mji wa Makambako Hususani katika Vizimba vya kuhifadhi taka ,Kuweni na tabia yakufanya usafi majumbani mwenu kwani msimu huu wa masika kuna wafanyakazi makazi yao ni machafu hivyo basi ni vema kwa idara ya mazingira kuzunguk pia hata katika makazi na maeneo wanayoishi watendaji na wafanyakazi
Hii itasaidia kuwa na mfano bora wa kuwahimiza wananchii na jamii kwa ujumla katika masuala ya usafi kwa wananchi ''Sitaki vizimba holela maeneo yasiyo rasmi watendaji simamieni usafi wa mitaa yenu hususani usafi ule ambao umewekwa kila mwisho wa mwezi lengo ni kuweka Mji wetu safi wakati wote.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa