Na. Lina Sanga
Mkurugenzi msaidizi wa uthibiti ubora wa elimu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia, Bi. Monica Mpululu amewapongeza wananchi wa Kijiji cha Mbugani,Kata ya Kitandililo kwa kutoa eneo lenye ukubwa wa ekari kumi, kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari ili kuwapunguzia umbali wanafunzi kuhudhuria masomo katika shule ya sekondari Mlowa na Kitandililo.
Mpululu alitoa pongezi hizo jana alipotembelea shule ya sekondari mpya ya Mbugani Kitandililo ikiwa ni ziara ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya BOOST na SEQUIP ambayo imefadhiliwa na benki ya dunia.
Amesema kuwa, wananchi waliotoa eneo hilo wameacha alama kwa vizazi vya sasa na vijavyo na kuwapongeza kwa jitihada za kuhakikisha wao wanapata elimu jirani na nyumbani na kuwataka kutunza miundombinu hiyo ili itumike muda mrefu pamoja na kuimarisha ulinzi wa watoto wa kike na kiume.
Reuben Swilla, Mratibu msaidizi wa mradi wa BOOST, Ofisi ya Rais TAMISEMI ametoa rai kwa jamii kuendelea kuhakikisha mahudhurio ya wanafunzi wa kiume yanaongezeka kwani idadi kubwa ya wanafunzi wanaoacha shule ni wanafunzi wa kiume,hali inayosababisha takwimu kuwa chini tofauti na wanafunzi wa Kike.
Julius Msigwa, kwa niaba ya wazazi wa wanafunzi katika shule hiyo na mmoja kati ya wananchi waliotoa eneo la ujenzi wa shule ameishukuru Serikali kwa ujenzi wa shule hiyo na kuahidi kuendelea kushirikiana na walimu kuhakikisha taaluma inakuwa na ulinzi wa mtoto unaimarika kwa kuhakikisha wanashughulikia matukio ya ukatili wa watoto yanayojitokeza.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Makambako, Ndg. Kenneth Haule ameishukuru benki ya dunia na Serikali ya awamu ya Sita kwa kuunga mkono jitihada za wananchi wa Kijiji cha Mbugani na Kitandililo kwa kutoa fedha za ujenzi wa shule hiyo, pia amewashukuru wananchi waliotoa eneo bila malipo kwa maslahi ya jamii na Watanzania kwa ujumla.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa