Na. Lina Sanga
Mbeya
Mkuu wa mkoa wa Katavi,Mhe. Mwanamvua Hoza Mrindoko ameipongeza Halmashauri ya Mji Makambako kwa kusimamia vema viwanda vilivyopo katika Halmashauri hiyo na kuhakikisha utambulisho wa bidhaa zinazozaliwashwa nchini unafanyika.
Mhe. Mwanamvua ametoa pongezi hizo leo,baada ya kutembelea na kukagua banda la Halmashauri ya Mji Makambako katika maonyesho ya nanenane yanayofanyika kitaifa viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya, na kushuhudia zao la parachichi kutoka Kiwanda cha AvoAfrica kilichopo mtaa wa Majengo katika Halmashauri ya Mji Makambako, ambacho hununua zao la parachichi kwa wakulima na kusafirisha nchi mbalimbali,kwa vifungashio vinavyotambulisha bidhaa hiyo kuwa ni mali ya Tanzania ingawa mmiliki wa kampuni hiyo ni mwananchi wa Kenya.
Amesema kuwa bidhaa nyingi zinazozalishwa nchini na kampuni za kigeni,huwekwa kwenye vifungashio vinavyotambulisha bidhaa zinazozalishwa nchini kwa majina ya nchi zingine kwa visingizio vya kukosa vifungashio nchini Tanzania.
"Hongereni sana kwa kusimamia vema viwanda vilivyopo katika Halmashauri yenu na kuhakikisha mali ghafi zote zinatambulika kuwa ni mali za Tanzania na sio nchi nyingine",alisema Mhe. Mwanamvua.
Aidha ameipongeza kampuni ya Lemi machinery Tachnologies kwa kuwa na zana nzuri za kilimo,ambazo zinamuwezesha mkulima kulima kilimo cha kisasa kwani zana hizo zinauzwa kwa bei rafiki na wakulima wadogo na wakubwa.
Pia amewapongeza wajasiriamali waliopo katika banda la Halmashauri ya Mji Makambako,kwa ubunifu wa bidhaa nzuri zenye tija kwa matumizi ya binadamu kama unga wa sembe wenye virutubisho kutoka kiwanda cha G2L na AKIAKI sembe,juisi ya misasati ambayo inasaidia kuongeza mmeng'enyo wa chakula, mvinyo wa nyanya,ufugaji wa samaki aina ya sato na kambale,ufugaji wa kuku aina ya kuchi ambaye kifaranga kimoja kinauzwa hadi shilingi elfu hamsini,ufugaji wa bata pamoja na unenepeshaji ng'ombe.
Ametoa wito kwa wamiliki wa viwanda wengine ambao wanatumia vifungashio vinavyotambulisha bidhaa za Tanzania kwa jina la nchi nyingine,kuacha mara moja na endapo hawana vifungashio vyenye utambulisho wa Tanzania watoe taarifa ili watengenezewe.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa