Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi Ruth Msafiri Pichani akizungumza na hadhara ambayo imekusanyika kwaajili ya kushuhudia uzinduzi wa gari la kubeba taka katika Halmashauri ya Mji wa Makambako zoezi ambalo limefanyika katika ofisi za Halmashauri ya Mji wa Makambako huku Mkuu wa wilaya ya Njombe akiwa kama mgeni rasmi wa shughuli hiyo .'Niwapongeze timu yote ya Halmashauri kwa kujitoa kufanya hiki ambacho kimetuweka hapa leo kwakweli ni furaha'.Amesema Mkuu wa Wilaya ya Njombe ,Ni vema tukaendana na kasi ya awamu ya tano chini ya Dk John Pombe Magufuli ya kujito kufanya kazi kwa ajili ya taifa letu tujitoe kwaajili ya maendeleo yetu .Katika sula la ununuzi wa gari amesema anategemea kuwa sasa Mji wa Makambako utakuwa safi na salama hali ambayo itafanya Halmshauri nyingine kuiga kutoka Makambako .suala la taka katika vizimba anategema kuona vizimba vinakuwa visafi kila siku kwani tayari kitendea kazi kipo .
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa