Pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Njombe ,Mhe Kissa Gwakisa Kasongwa ambaye amefanya mazungumzo na watumishi wa Makao Makuu ya Halmashauri ya Mji wa Makambako kwa lengo la kujua nini kinafanyika ,hasa katika idara mbalimbali za Halmshauri ya Mji wa Makambako.
Mkuu wa wilaya amesomewa ripoti ya kazi za idara mbalimbali kwa mwaka wa fedha 2020/ 2021 kwa Halmashauri ya Mji wa Makambako taarifa ambayo imesomwa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Makambako Bi .Appia Mayemba.
Mara baada ya kusikiliza taarifa hiyo Mkuu wa wilaya ya Njombe amepongeza ingawa taarifa kwa baadhi ya idara zimeandikwa kwa ufupi sana ukilinganisha na ukubwa wa idara hizo Mfano idara ya fedha na idara ya kilimo na Mifugo, kwa idara ya Kilimo: Ni idara ambayo Inatakiwa ichakatwe kwa kina kwani inabeba Mkoa wa Njombe katika masuala mazima ya kilimo kwa nyanda za juu Kusini mwa Tanzania ,Katika Idara ya fedha pia Mkuu wa Wilaya amegusia suala la mapato kuwa, taarifa hairidhishi kutokana na Halmashauri ya Mji wa Makambako kuwa lango la Mkoa wa Mjombe hivyo mapato yalitakiwa yawe juu zaidi kushinda Halmshauri zote zinazounda Wilaya Njombe yaani Halmashauri ya wilaya ya Njombe na Halmashauri ya Mji wa Njombe.
Aidha Mkuu wa wilaya ametoa agizo kwa wakuu wa idara zote ,Idara ya ujenzi wakati wa ukaguzi wa miradi Nyaraka zote za ujenzi wa mradi husika ziwe katika mpangilio na weledi mkubwa ili aweze kuelewa nini kimefanyika na sheria na kanuni zinafuatwa? pia kwa idara ya Maendeleo ya Jamii fedha kwaajili ya Wanawake,Vijana na watu wenye mahitaji maalumu,Je zinawafikia kwa wakati muafaka?na Kwa idara ya Elimu watoto lazima wapate chakula cha mchana mashuleni hiyo ni lazima wazazi wakumbushwe kuwa kuchangia michango ya chakula ni lazima kwa watoto wao .Akihitimisha Mazungumzo hayo Mkuu wa wilaya ametoa agizo kwa watumishi hasa sehemu zao za kazi kufanya kazi kwa ushirikiano na upendo bila kujali mtu ,kabila na hata rangi kwani sote tupo kwaajili ya nchi yetu kwa ujumla kuzingatia muda wa kazi, kuwepo kazini masaa ya kazi na matumizi sahihi ya lugha kwa Watu tunaowahudumia ni jambo la msingi.Pia Mkuu wa wilaya ameahidi kufanya ziara za kushitukiza katika sekta mbalimbali hasa sekta ya Afya, Elimu, Maji na Umeme lengo ni kutaka kuimarisha utendaji kazi kwa watumishi wote.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa