Na. Lina Sanga
Taarifa hiyo imetolewa na Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Dkt, Tulia Ackson leo alipokuwa akizungumza na wakazi wa mji wa Makambako, waliposimamisha Msafara wake wakati akielekea Mkoani Mbeya leo.
Dkt. Tulia amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Suluhu Hassan amewapunguzia Mzigo wazazi wa Mkoa wa njombe kwa kujenga madarasa pasipo kuwachangisha fedha.
“Miradi mingi Mhe. Rais amefanya kwa leo nitaje miradi miwili,moja ni huu mradi wa zaidi ya Bil. 15 ambao Mhe. Waziri mkuu atakuja hapa kuzindua Mradi wa kiwanda cha dawa,sasa jamani sisi Njombe pekee yetu tu kiwanda namna hiyo,na huko kwingine vipo lakini sisi tunaongea yetu ya Njombe hata ninyi wananchi mashahidi,lakini pia sisi wazazi tulikuwa tunachangishwa fedha ili watoto wetu mwezi wa kwanza waingie madarasani lakini safari hii madarasa yamejengwa tena yakiwa na madawati”, alisema Dkt. Tulia.
Ametoa wito kwa wananchi wote wa Mkoa wa Njombe kujitokeza kwa wingi,pindi Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atapotembelea Mkoa wa Njombe, na kumueleza miradi yote iliyotekelezwa yenye ubora na hata isiyo na ubora, lakini pia kutoa kero na mapendekezo yao kwa wabunge wao ili waweze kufikisha bungeni na kufanyiwa kazi.
Pia Dkt. Tulia ametoa shukurani kwa Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Wakazi wote wa Mkoa wa Njombe kwa Upendo wao kwake na Wabunge wa majimbo yote yaliyopo Mkoa wa Njombe,kwani asilimia mia moja alizopata na wao wamechangia ushindi na hatimaye kuibuka mshindi wa kiti cha Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa