Na. Lina Sanga
Njombe
Tamko hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka januari 5,mwaka huu katika mkutano wa saba wa baraza la biashara Mkoa wa Njombe na kuwataka wazazi kukamilisha mahitaji yote muhimu ya watoto ili waanze masomo kwa mujibu wa ratiba, na kutoa onyo kwa wafanyabiashara wanao ongeza bei ya mahitaji ya wanafunzi kiholela kuacha mara moja.
Mhe. Mtaka amesema kuwa, wapo baadhi ya watoto hawana uwezo wa kupata mahitaji ya shule kutokana na hali duni ya maisha katika familia, lakini amepata ufaulu mzuri wa kuendelea na masomo na wengine wamefikia umri wa kuanza elimu ya awali na msingi lakini hawana uwezo wa kupata sare za shule hivyo Mkoa una jukumu la kuhakikisha watoto hao wanapata elimu bila kikwazo.
"Nyumba za nyasi zimetoa maprofesa wengi na baadhi ya nyumba za ghorofa zimetoa matahira, hivyo ni wajibu wa Mkoa,Halmashauri na Wadau wa maendeleo katika Mkoa wa Njombe kujitoa kwa ajili ya kuwawezesha watoto wa masikini kupata elimu kwa kuwasaidia mahitaji muhimu ya shule",alisema Mhe. Mtaka.
Ametoa wito kwa walimu wakuu wa shule zote katika Mkoa wa Njombe kuwapokea watoto wasio na sare za shule ili waanze masomo yao kwa mujibu wa ratiba ya masomo , Mkoa na Halmashauri zitawatambua watoto hao shuleni na kuwakamilishia mahitaji yao kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo.
Aidha,ametoa angalizo kwa Walimu Wakuu kutoweka masharti magumu ya wanafunzi wanaotakiwa kuanza masomo,kwa kumlazimisha mzazi kununua sare za shule zaidi ya moja kwa kutozingatia hali halisi ya kiuchumi ya mzazi na kusababisha baadhi ya wanafunzi kutopokelewa shule au kutofika shuleni kwa kutotimiza masharti yaliyopo kwenye fomu ya maelekezo ya kujiunga na shule.
Pia, amewataka wazazi kukamilisha mahitaji ya watoto wao na Serikali haitasita kuwachukulia hatua wazazi watakao shindwa kuwatimizia mahitaji watoto kwa uzembe.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa