Na. Tanessa Lyimo
Jumla ya nyumba Kumi na mbili katika Kata ya Lyamkena Halmashauri ya Mji Makambako zimepata majanga ya kuezuliwa paa ,kubomoka kuta na kuleta uharibifu wa chakula kufuatia mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha Januari 3,2025 majira ya saa nane mchana katika Mtaa wa Ikwete na Malombwe.
Kamati ya maafa ya Halmashauri ya Mji Makambako imetembelea na kufanya tathmini ya athari zilizojitokeza ambapo kijana mmoja anayeitwa Eliah Kapuge (15),mkazi wa Mtaa wa Ikwete alijeruhiwa na tayari alipatiwa matibabu na ananendelea vizuri na hakuna taarifa ya kifo kilichotokea.
Wakiongea na Kamati ya Maafa Mwenyekiti wa Mtaa wa Malombwe na Mtaa wa Ikwete Bw. Daniel Japhet na Amon Ernest wameishukuru uongozi wa Halmashauri pamoja na diwani wa Kata ya Lyamkena Mhe. Salum Mlumbe na wadau mbalimbali katika kusaidia wananchi waliopatwa na Maafa hayo.
Uongozi wa Halmashauri ya Mji Makambako unawapa pole wananchi wote waliofikwa na majanga hayo na kuwataka kuwa na Subira wakati hatua mbalimbali za kiutawala zikifanyika , lakini pia unawashukuru wasamaria wema waliojitolea kuwahifadhi wahanga waliokosa makazi.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa