Pichani ni katibu tawala wilaya ya Njombe akizungumza na wananchi pamoja na watendaji katika Halmashauri ya Mji wa Makambako ,Lengo likiwa ni kuwakumbusha na kuwahimiza watendaji kuwa kazi na majikumu kama wafanyakazi yanaendeea kama kawaida .Hii ni mara baada ya kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa awamu ya Tano Hayati Dk John Pombe Magufuli baadhi ya wananchi na jamii kwa ujumla wamekua wakiulizana nchi itaendaje au nani ataongoza na hata wengine kuwa na wasiwasi mkubwa juu ya mustakabali na maendeleo ya nchi ka ujumla.
Watendaji na watumishi watoeni wananchi hofu kuwa inchi itaenda vipi na maswali ya hapa na pale kwani tayari tunaye Rais Mama Samiah Suluhu Hassan na timu yake kubwa tuwe na imani yakuwa inchi itafika pale inapotakiwa acheni kukata tamaa na kua na maswali ambayo yatawarudsha nyuma kwani kifo kipo na kuna maisha yanaendelea kwa ambao tupo hai.
Shirikianeni katika kufanya kazi pendaneni acheni tabia ya kuwa kila mtu afanye kazi kivyake ,kwani kuna mambo mengine yanashindwa kusonga kwasababu mtu fulani anamaslahi yake binafsi sisi sote ni watanzania tufanye kazi kwa upendo ili tuweze kufika mbali katika nyanja mbalimbali hususani katika masuala mazima ya kiuchumi ,kisiasa na hata kimtizamo
Katibu tawala hakuacha kugusia suala lawatumishi katika sekta ya afya kwani kumekuwepo na maneno kutoka kwa wananchi juu ya huduma zenu bado kuna shida ,Niwaombe fanyeni kazi kwa weledi ,umakini na upendo acheni Rushwa ,Tamaa ,Maslahi yasiyo na msingi pia simamieni matumizi sahihi ya dawa mtaepukana na lawama kwa wananachi vinginevyo mjitafakari katika masuala mazima utoaji huduma kwa jamii
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa