Katika picha ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Makambako Keneth Haule akizungumza na wafanyakazi makao makuu ya Halmashauri ya Mji wa Makambako lengo likiwa ni kukumbushana masuala ya kazi mara baada ya Mkurugenzi aliyekuwepo kuhamia buchosa Mkoani Mwanza.
Awali akizungumza na wafanyakazi amesema hakuna kitu kilichobadilika kwake kwani wakuu wa idara wapo wafanyakazi wapo labda mazingira kwake ni tofauti kule alikotoka ni Handeni huku ni Makambako lakini si kiutendaji kwakuwa zote ni serikali za mitaa.
Haule amesema kuwa wafanyakazi wanapaswa kukumbuka kuwa wapo kwaajili ya kuwatumikia wananchi na si vinginevyo "SIPENDI UBABAISHAJI" katika kazi tufanye kazi kwa weledi,Taaluma na maadili ya utumishi wa umma katika mazingira ya kazi si vinginevyo."Wapo baadhi ya watumishi hujiona wao kama Mungu watu tambueni kuwa mpo kwaajili ya wananchi kwa kuwasaidia,kuwapa huduma bora acheni kufanya kazi kwa zima moto ,kufanya kazi kwa kumfurahisha mtu au ili uonekanae kwa mtu fulani bali fanya kazi kwaaji ya Watanzania wote''.
Ameongeza kuwa ipo tabia ya kuchelewa kutoa huduma kwa wananchi kwani wapo wananchi ambao wanafika mapema katika ofisi kwa lengo la kupata huduma lakini unakuta mfanyakazi anampiga kalenda nyingi mhudumiwa;Mfano njoo kesho njoo keshokutwa ,mara mkuu wa idara hayupo ,anumwa hali hii inawafanya wananchi kukosa uaminifu na uadilifu wa kazi kwa watu mnaowapa huduma .
Pamoja na kugusia suala la kuchelewa kuwapa huduma wananchi amegusa Matumizi ya lugha za kuwahudumia wananachi kwaujumla "Acheni lugha zinazokatisha tamaa kwa watu mnao wahudumia hasa lugha za kejeli ,fedheha ,matusi na lugha zote ambazo zitawafanya watu kukosa imani na utendaji kazi wenu pamoja na serikali kwa ujumla na kwa mantiki hiyo kazi zifanywe kwa wito kutokana na taaluma zenu na weledi mkubwa kwani kwa kufanya hivyo wananchi na jamii kwa ujumla imani kubwa kwenu na serikali inayowaongoza itaongezeka.
Aidha Mkurugenzi amesema kuwa ni vema wafanyakazi wakatambua kuwa wamewekwa kwaajili ya wananchi na taaluma zao ziwe na tija kubwa kwa watu wanao wahudumia bila kujali lugha ,dini, kabila jinsia na hata rangi kwani mfanyakazi aliye na wito na kazi yake atajisikia fahari kubwa hudumia jamii yake kwa lugha nzuri yenye ufasaha na yenye kuleta upendo kati ya mhudumu na mhudumiwa kwakuwa haina haja kutumia lugha ambazo zitaweka maswali yasiyo na majibu ,zitaweka kigugumizi na kuleta chuki kati yetu tukumbuke sisi sote ni watanzania .
Suala la muda wa kufika na uondoka kazini limetizamwa kwa jicho la tatu na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Makambako ambapo amewasihi wafanyakazi kujitafakari kwa weledi katika matumizi ya muda wa ofisini kwa kufuata sheria na taratibu za utumishi wa umma hasa kwa muda wa kufika na kuondoka ofisini,Amesema kwa kawaida ofisi zote za serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania muda wa kufika ofisini ni saa moja na nusu na muda wa kuondoka ofisini ni saa tisa na nusu si kinyume na hapo.
Akimalizia nasaa za kikao hicho kifupi amegusa utunzaji wa mali na thamani za serikali kwa kuwaambia wafanyakazi kuwa ukitunza mali iliyopo sasa hata watoto wako watakuja kutumia kwani ni aibu kuwa na mtumishi ambaye hana uzalendo na thamani za serikali hali hiyo itaandaa kizazi ambacho hakina uzalendo na mali za serikali ''Tunzeni mali hizo kwa ajili ya vizazi vya baadae".Mfano katika shule madawati yatunzwe vizuri ,Hospitali pia miundo mbinu itunzwe vizuri na sehemu yoyote ili itumike hata kwa vizazi vijavyo.
"Nitegemee Uzalendo, Ushirikiano kwa idara zote za Halmshauri ya Mji wa Makambako na KAZI IENDELEE.Asiyefanya kazi asile "Kenethi Haule Mkurugenzi Halmashauri ya Mji wa Makambako.''
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa