Na. Lina Sanga
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka amewapongeza wanufaika wa TASAF katika Halmashauri ya Mji Makambako, kwa kuupokea mradi wa parachichi na kuzihudumia vizuri licha ya baadhi yao kukabiliwa na ukosefu wa Maji.
Mhe. Mtaka alitoa pongezi hizo jana katika ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya mradi huo, ambao ulianzishwa kwa ajili ya kuwajengea uchumi endelevu wanufaika hao ili kukuza pato la familia na lishe katika kaya zao.
Amesema kuwa, jitihada za wanufaika hao kuongeza idadi ya miti ya parachichi baada ya Serikali kuwagawia miche 10 zinaonyesha dhahiri uhitaji wa mradi huo hivyo changamoto ya maji inatafutiwa ufumbuzi.
“Mimi nawapenda na nawapenda sana kwa namna ambayo mmesaidia mradi kutokea,hili la maji tutazungumza na Mkurugenzi tuone tunafanyaje kwa sasa tuandae vizuri maeneo yetu kwa kuweka mbolea ili mvua ikinyesha ikute chakula kipo tayari kwenye parachichi, mpaka mvua itakapo isha mi naamini mwakani tutaanza kupata matunda”,alisema Mhe. Mtaka.
Amemtaka mratibu wa TASAF katika Halmashauri ya Mji Makambako kuwatambua mabinti wanaowatunza wazee ambao ni wanufaika wa TASAF, ili waandikishwe na kuwezeshwa mitaji katika shughuli wanazozifanya ili wawatunze vizuri babu na bibi zao.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa