Na. Lina Sanga
Njombe
Kauli hiyo imetolewa na Mhe. Waziri Kindamba ambaye alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe na sasa ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe,alipokuwa akizungumza na Viongozi wa dini,viongozi wa mila,viongozi mbalimbali wa Serikali na wananchi wa Mkoa wa Njombe waliohudhuria Kongamano la kuiombea Nchi ya Tanzania na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Suluhu Hassan,lililofanyika leo Mkoani hapa.
Mhe. Kindamba amesema kuwa ni ngumu sana kusema kwa heri kwa wananchi wa Mkoa wa Njombe,lakini hana budi ya kuaga na kwenda kutumika katika kituo kipya cha Kazi na kuahidi kuendelea kushirikiana na wana Njombe kwa mambo mbalimbali.
Amesema kuwa,wananchi wa Njombe wana upendo uliopitiliza usio wa kinafiki na walimpokea kwa upendo pasipo kujali dini yake wala kabila,kwani viongozi wa dini na kimila wote walimpokea kwa upendo wa dhati na hawakumbagua.
Ameongeza kuwa wananchi wa Njombe pia wanapenda kazi pasipo kusukumwa licha ya hali ya hewa ya baridi lakinbi bado wanajituma katika kufanya kazi,pia ni watiifu na wanyenyekevu wa mamlaka za Serikali hivyo Njombe imemfundisha mengi sana na atayaishi yote aliyojifunza Njombe na yupo tayari kurudi tena Njombe.
Ametoa rai kwa wananchi wa Njombe kuendelea kuwa na mshikamano na kumpa ushirikiana mkuu wa mkoa anayekuja na kuendelea kusonga mbele kwa ari na moyo mkuu pasipo kurudi nyuma,na kuwatumia wazee katika ushauri wa masuala mbalimbali pamoja na kujifunza busara mbalimbali.
Mwisho amewakaribisha wananchi wote wa Mkoa wa Njombe Mkoani Songwe na kushirikiana katika masuala mbalimbali,pia amemshukuru Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kumuamini na kumpa nafasi nyingine ya kulitumikia taifa na kwa upendo wake na uzalendo wake wa kuwezesha na kuboresha mazingira ili wananchi wa Tanzania waendelee kuishi kwa usalama,amani na ustawi mzuri.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa