Na. Lina Sanga
DODOMA
Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Mhe. Innocent Bashungwa katika kikao kazi na Maafisa habari wa Mikoa,Halmashauri na Taasisi zilizopo chini ya Ofisi ya Rais TAMISEMI, kilichofanyika leo jijini Dodoma katika Ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Wa Dodoma.
Bashungwa amesema kuwa licha ya umuhimu wa habari kwa Umma kuna baadhi ya wakurugenzi na wakuu wa taasisi wanachukulia poa kazi za maafisa habari,hali inayokwamisha utoaji wa taarifa kwa wananchi kuhusu kazi zinazofanywa na Serikali.
"Maafisa habari ni daraja kati ya Serikali na wananchi kwa kutoa habari za kazi kubwa zinazofanywa na Serikali nchini na kazi anayofanya Mhe. Samia Suluhu Hassan na Serikali ya awamu ya sita lakini nasikitishwa licha ya maagizo mbalimbali yaliyotolewa kwa wakurugenzi bado wapo wanaopuuza na kukwamisha kitengo cha habari kufanya kazi zake",alisema Bwashungwa.
Ametoa angalizo kwa Wakurugenzi wote wanaochukulia poa kazi za Kitengo cha mawasiliano Serikalini kuacha mara moja na atayekaidi atachukuliwa hatua stahiki kwani haki ya wananchi kupata habari ni ya kikatiba na ni lazima wananchi wapate habari.
Pia amewataka Maafisa habari wote kutekeleza wajibu wako katika nafasi zao ili haki na wajibu ziende sambamba,pamoja na kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali katika Halmashauri na taarifa za kukanusha upotoshaji mbalimbali unaotolewa kwenye mitandao ya kijamii unaoanzia katika maeneo yao ya kazi.
Aidha, Bashungwa ametoa agizo kwa Katibu Mkuu kukaa na Wakurugenzi na kutatua changamoto ya vitendea kazi kwa vitengo vya mawasiliano kupitia bajeti maalumu,pamoja na kufanya msawazo wa Maafisa habari ili kila Mkoa na Halmashauri iwe na Afisa habari ili kupata upungufu halisi wa Mahitaji ya Maafisa habari kila Halmashauri na Mkoa.
Jumla ya Mikoa 4 haina maafisa habari kati ya mikoa 26 na Halmashauri 118 hazina maafisa habari kati ya Halmashauri 184,Katika kukabiliana na upungufu wa Maafisa habari jumla ya Maafisa 38 wameajiriwa na baada ya msawazo huenda idadi ya upungufu itapungua zaidi.
#jiandaekuhesabiwa2022
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa