Na. Lina Sanga
Mbeya
Wizara ya ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) pamoja na watumishi wote waliopo chini ya Wizara hiyo,hawatakuwa tayari kumuangusha Mhe. Samia Suluhu Hassan katika dhamira yake ya kuendelea kufanya mapinduzi makubwa katika sekta ya Kilimo.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa leo, alipokuwa akitoa salamu kwa Mhe. Samia Suluhu Hassan katika kilele cha maadhimisho ya nanenane viwanja vya John Mwakangale Mkoani Mbeya.
Mhe. Bashungwa amesema kuwa Mzigo unaotakiwa ubebwe na mama husaidiwa na vijana,hivyo Wizara ya OR-TAMISEMI pamoja na Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya watajipanga kusimamia vyema mabilioni ya fedha,zilizotolewa kwa ajili ya wakulima ili waweze kujikwamua kimaisha kupunguza gharama za maisha na kufanya uzalishaji mkubwa kwa maendeleo ya nchi.
Amesema kuwa kuhusu wakulima hewa ambao hufanya udanganyifu ili kupata mbolea ya ruzuku, Wizara ya OR-TAMISEMI itashirikiana na Wizara ya Kilimo kuhakikisha mbolea hiyo inawafikia walengwa.
Ametoa shukurani kwa Wizara ya Kilimo kwa kutoa pikipiki 2,500 Kwa Maafiaa Ugani, mashine za kupimia udongo, na kutenga bajeti kwa ajili ya ununuzi wa pikipiki zingine katika bajeti ya mwaka 2022/2023.
Pia ametoa shukurani kwa Naibu Katibu wa Mifugo na Uvuvi kwa kutoa pikipiki 300 kwa maafisa ugani.
Ametoa maelekezo kwa Wakuu wa Mikoa,Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri, kuhakikisha vitendea kazi vilivyotolewa kwa ajili ya maafisa ugani kama pikipiki vinatumika kwa malengo yaliyokusudia pamoja na kusimamia mabilioni ya Fedha zilizotolewa kwa ajili ya Wakulima.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa