Na. Lina Sanga
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka ameipongeza TASAF kwa kuibua miradi inayoishi kwa ajili ya wanufaika wa TASAF ambayo itawawezesha kuwa na kipato endelevu kupitia miradi hiyo.
Mhe. Mtaka ametoa pongezi hizo leo katika Kijiji cha Ikelu, Kitongoji cha Nyambogo kabla ya kuwakabidhi wanufaika 27 mradi wa ng’ombe wa Maziwa,ili kuwawezesha kuwa na kipato endelevu na kuboresha lishe ya Kaya.
Amesema kuwa, kupitia ng’ombe hao wanufaika hao watakuwa na uhakika wa kupata shilingi 10,000 kwa siku,shilingi 300,000 kwa mwezi na mil.3 kwa mwaka kupitia ng’ombe mmoja kwa kuuza maziwa na kupata faida kwa kuuza ndama.
Ametoa rai kwa TASAF na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Makambako, kununua mashine ya kusaga mabua ili kuwawezesha wanufaika kutengeneza chakula cha ng’ombe, kwani mradi huo una tija kubwa kwa wanufaika hao.
Naye, Mratibu wa TASAF Mkoa wa Njombe, Bw. Mussa Selemani ametoa rai kwa wanufaika waliokabidhiwa ng’ombe kutunza ng’ombe hao ili kufikia malengo, na wanufaika watakaoshinda kutunza mradi, TASAF haitasita kuhamisha na kukabidhi Kaya nyingine.
Jumla ya wanufaika wa TASAF 27 wamekabidhiwa ng’ombe wa maziwa ambapo mradi huo unagharimu mil. 30.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa