Na. Lina Sanga
Njombe
Sekta ya Maliasili na utalii inachangia pato la taifa kwa asilimia 17.5 na fedha za kigeni asilimia 25,pamoja na kutoa ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja Mil 1.5.
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe. Mary Masanja (Mb) katika hafla ya uzinduzi wa mikakati ya kutangaza utalii kusini mwa Tanzania,iliyofanyika leo katika Ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Mji Njombe.
Mhe. Masanja amesema kuwa kwa mujibu wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),kuitaka sekta ya Maliasili na utalii ifikapo mwaka 2025 kuongeza kiwango cha watalii kutoka mil 1.5 hadi mil. 5.
Amesema kuwa, kupitia uzinduzi wa mikakati ya kutangaza vivutio vya utalii mikoa ya Kusini itasaidia kufikia lengo la kuongeza watalii kama inavyoelekeza ilani ya Chama Cha Mapinduzi.
Ametoa rai kwa wakuu wa mikoa kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo kwenye mikoa yao,ili kuinua uchumi wa wananchi katika maeneo hayo kwani sekta ya utalii ni eneo muhimu sana,na ina uwezo wa kuongeza uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na kuchangia pato la taifa.
Ametoa wito kwa wadau wa utalii na wananchi wa miko ya kusini kwa ujumla,kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kufanya utalii wa ndani baada ya shughuli mbalimbali kwa ajili ya mapumziko.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa