Na. Lina Sanga
Kaimu meneja wa Mamlaka ya kuhifadhi Chakula Nchini (NFRA),Frank Felk amesema kuwa kumekua na utaratibu wa kuuza mahindi kila baada ya miaka mitatu na kuanza kubadilika rangi na kuwauzia watu walioomba kupitia makao makuu.
Frank alitoa kauli hiyo jana katika mkutano wa baraza la Madiwani la robo ya tatu uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya Mji Makambako,kutokana na madai ya baadhi ya wananchi kuwa Serikali inauza mahindi kwa nchi jirani licha ya tishio la uhaba wa mahindi mwaka huu kutokana na uhaba wa mvua baada ya kushuhudia malori yakipakia tani kadhaa za Mahindi kutoka kwenye maghala ya kuhifadhia Chakula yaliyopo Mjini hapa.
Amesema kuwa ni utaratibu wa kawaida kuuza mahindi yaliyohifadhiwa kwa miaka mitatu na mahindi yanayotolewa sasa yalinunuliwa mwaka 2018,mpaka sasa tani 2000 bado kumalizia zoezi la kutoa mahindi ya zamani na kubakiza mahindi mapya.
Naye mwenyekiti wa halmashauri ya Mji Makambako, Mhe. Hanana Mfikwa ametoa wito kwa wananchi kuhifadhi chakula baada ya mavuno ili kuepukana na janga la njaa,ambalo linaweza tokea kutokana na mvua hafifu iliyonyesha na kusababisha mazao kukauka.
Pia ametoa angalizo kwa shule zote kuhakikisha chakula cha wanafunzi,kinapatikana kwa kuanza kukusanya mapema.
#jiandae kuhesabiwa
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa