Na. Lina Sanga
Jumla ya bil. 17 kutolewa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya ukamilisha wa ujenzi wa kiwanda cha dawa na vifaa tiba kilichopo idofi,Kata ya Mlowa katika Halmashauri ya Mji Makambako.
Taarifa hiyo imetolewa na Mhe. Ummy Mwalimu,Waziri wa Wizara ya Afya alipokuwa akitoa salamu kwa wakazi wa Halmashauri ya Mji Makambako leo,waliofika kumsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Mhe. Ummy amesema kuwa,ujenzi wa kiwanda hicho kwa sasa umesimama kutokana na mambo mbalimbali,lakini ujenzi wa kukiendeleza na kukikamilisha kiwanda hicho unatarajiwa kuanza pindi kiwanda hicho kikikamilika kitazalisha dawa za vidonge,dawa za maji na glovu na kitazalisha jumla ya ajira 200 ambazo wanufaika wakubwa ni kina mama na vijana waishio Makambako..
Pia,amesema kuwa kipaumbele cha Mhe, Samia ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya na sio bora huduma,hivyo sambamba na majengo Wizara kwa sasa inaangalia muda ambao mwananchi aliotumia kupata huduma,upatikanaji wa dawa,vipimo pamoja na lugha za watumishi wa sekta ya afya,upatikanaji wa huduma ya bure kwa wazee wasio na uwezo na kupunguza gharama za matibabu kwa wananchi.
Ameongeza kuwa,ili kutoa huduma bora kwa wananchi Wizara ya afya na Wizara ya OR-TAMISEMI,zimetoa magari mawili ya wagonjwa(Ambulance) kwa Halmashauri ya Mji Makambako,na magari hayo yameshafika bandarini.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa