Na. Lina Sanga
Tamko hilo limetolewa leo na Waziri wa elimu,sayansi na teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda katika Mkutano wa hadhara Kata ya Lyamkena,mara baada ya Mbunge wa jimbo la Makambako, Mhe. Deo Sanga kuhoji hatima ya Makambako kupata chuo cha ufundi (VETA) au shule ya ufundi,kwani eneo lilishatengwa tayari bado utekelezaji.
Mhe. Prof. Mkenda amesema kuwa, katika mapinduzi ya elimu Serikali ina mpango wa kujenga shule za sekondari 100 za amali ya ujuzi ili kuwawezesha wanafunzi kujifunza fani mbalimbali kama ufundi,mziki na kilimo ili kuwawezesha kujiajiri na Makambako itajengwa shule moja ya mchepuo wa ufundi mbalimbali ili wanafunzi wajifunze masuala ya kama ufundi magari na umeme sambamba na kujifunza masomo ya biashara na ujasiriamali.
Pia, amepongeza na kuzindua wodi pacha katika kituo cha Afya Lyamkena na ujenzi wa madarasa katika shule ya Msingi Magomati iliyopo Kijiji cha Usetule katika Kata ya Mahongole na kuahidi kufikisha ombi la gari la kubebea wagonjwa kwa ajili ya Kituo cha Afya Lyamkena.
Naye,Bw. Christian Nyagenda Mkazi wa Mtaa wa Lyamkena ameishukuru Serikali kwa kujenga Kituo cha Afya katika Kata ya Lyamkena na kusogeza huduma kwa wananchi kwani uwepo wa vituo vya Afya na Zahanati kila Kata unapunguza msongamano wa wagonjwa wanaohitaji huduma.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa