Wanafunzi wa shule ya sekondari Mtimbwe wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Njombe katika ufunguzi Rasmi wa Bweni la wavulana katika shule hiyo ,Ambapo Mkuu wa wilaya aliwasihi Wanafunzi kutumuia muda wao mwingi kujisomea na kufikiri zaidi masuala ya kitaaluma na zaidi kuepuka vishawishi vinavyoweza kuharibu ndoto zao za baadae .Aidha walimu pia amewakumbusha kuacha Masuala ya ushabiki wa siasa mda wa kazi badala yake watumie muda mwingi kuwasaidia watoto hao kwani ndio Madaktari ,Wanajeshi,,Marubani ,Wahandisi na Walimu wa kesho .Shule ya sekondari mtimbwe ni moja kati ya shule 10 za serikali zilizopo ndani ya Halmashauri ya mji Makambako yenye jumla ya wanafunzi 583 kati yao wavulana ni 337 Na Wasichana ni 346 na walimu 30 .Katika ujenzi wa bweni la wavulana lilifunguliwa Rasmi na mkuu wa wilaya ya Njombe asilimia 90 ni fedha toka mradi wa TASAF ambayo ni sawa na shilling 70,448,330.79 na mchango wa Wananchi ni 10 asilimia ambayo ni sawa na shilling 7,470,000.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa