Na. Lina Sanga
Mkuu wa Mkoa wa Njombe,Mhe. Anthony Mtaka ametoa kauli hiyo leo baada ya kusikiliza kero na changamoto wanazopitia walimu,pindi wanapohitaji huduma katika ofisi za Halmashauri hasa idara ya utumishi.
Mhe. Mtaka amesema kuwa ipo haja ya kufanya vikao pamoja timu ya menejimenti na watumishi katika Halmashauri zote za Mkoa wa Njombe,ili kuhakikisha kila Mkuu wa idara anawajibika kwa nafasi yake pamoja na uimara wa timu ya menejimenti wa kushughulikia masuala ya utumishi.
Amesema kuwa timu ya menejimenti inabeba dhamana ya watumishi ndiyo maana Mkurugenzi wa Halmashauri ni Muajiri na vitambulisho vya watumishi vina muhuri wake na kikao na watumishi wa idara ya utumishi kitafanyika kuwekana sawa.
"Tutafanya kikao na watu wa utumishi kuwekana sawa,niwahakikishie walimu hayo ni masuala madogo sana,kwa sababu mimi naamini ili tuweze kufanikiwa kwenye agenda tunazokubaliana ni lazima manung'uniko yaliyo ndani ya uwezo wetu tuweze kuondokana nayo",amesema Mhe. Mtaka.
Ametoa rai kwa watumishi wa idara ya utumishi kushughulikia masuala mbalimbali ya watumishi,kwani nafasi hizo sio za kudumu endapo mtumishi anatakiwa kupandishwa daraja hawana budi kumpandisha kwani fedha sio zao.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa