Na. Lina Sanga
Kamati ya Fedha na Uongozi ya Halmashauri ya Mji Makambako imeunga mkono mapendekezo ya miradi itakayopitiwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024,na kuagiza mradi wa soko la mazao la kiumba kuwa mradi namba moja kwani ni mradi wa Halmashauri na sio Serikali Kuu.
Kamati ya Fedha na Uongozi imetoa rai hiyo leo katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika kipindi cha kuishia robo ya tatu kwa mwaka wa fedha 2023/2024, na kuiagiza timu ya menejimenti kuhakikisha mwenge wa Uhuru unazindua soko hilo na si vinginevyo.
Mhe. Hanana Mfikwa ,Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Makambako amesema kuwa, katika Mbio za Mwenge kwa mwaka huu Halmashauri ya Mji Makambako ina miradi miwili ambayo ni soko la kiumba na madarasa mawili yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi katika shule ya sekondari ya Mbugani-Kitandililo,miradi mingine ni ya Serikali kuu,hivyo Halmashauri inajivunia kuwa na miradi miwili ambayo itazinduliwa na kuwekwa jiwe la msingi na Mwenge,ikiwa ni miradi ambayo baraza la madiwani ilibariki utekelezaji wake.
Amesema kuwa, Halmashauri imewekeza zaidi ya mil. 300 kwa kulipa fidia maeneo hayo, na wananchi wamewekeza zaidi ya bil. 1 katika ujenzi wa maghala na vizimba , na ujenzi wa soko hilo ulifuata hatua zote kisheria ,hivyo Kamati ya fedha na Uongozi haipo radhi kupoteza fedha hizo pasipokuwa na sababu za msingi,kwani Mji unatakiwa kupangwa na kuendelezwa kwa maslahi ya Umma.
Kamati ya Fedha na Uongozi imetoa wito kwa kamati za Mwenge za Wilaya na Mkoa kutouondoa mradi huo na kuitaka timu ya menejimenti na TARURA kuendelea kufanya maboresho ya miundombinu ya soko kama ilivyoagizwa awali.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa