Na. Lina Sanga
Tamko hilo limetolewa leo na Afisa Biashara,Viwanda na Uwekezaji wa Halmashauri ya Mji Makambako,Bw. Carlos Mhenga katika kikao na baadhi ya Viongozi wa wafanyabiashara wa mazao katika Mji wa Makambako.
Mhenga, alitoa tamko hilo mara baada ya kupokea malalamiko ya baadhi ya wafanyabiashara wa mazao ambao bado hawajahamisha stoo zao zilizopo katika makazi ya watu,pembezoni mwa soko kuu la Makambako kwa madai ya kutokuhama endapo wauza mazao waliopo soko kuu hawatabaki.
Mhenga,amesema kuwa wafanyabiashara wa mazao katika soko kuu la Makambako wapo kihalali ,kwani soko hilo linatoa huduma ya bidhaa mchanganyiko ikiwa ni pamoja na nafaka ambazo hazizidi gunia tano,na wafanyabiashara hao hawatibu mazao yaliyopo sokoni bali yaliyopo stoo,ambazo zilikuwa katika makazi ya watu na walishapewa maeneo ya kujenga stoo katika soko la Kiumba.
Naye Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai Kituo cha polisi Makambako,OCCID Gotfrid Kimboy ,kwa niaba ya Mkuu wa polisi Wilaya ya Kipolisi Makambako,amewataka wafanyabiashara hao kutii agizo kwani mpaka Serikali imeratibu ujenzi wa soko hilo ushirikishwaji ulikuwepo,na jeshi la polisi lipo kusimamia utekelezaji wa kazi na maagizo ya Serikali.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa