Na Tanessa Lyimo
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Makambako Ndg. Keneth Haule amewataka wananchi kutambua umuhimu wa Usafi wa mazingira katika Mji ni jukumu la kila mwananchi katika jamii, hivyo hawana budi ya kujenga utamaduni na desturi ya kufanya usafi kwa kutotupa taka ovyo au kutirisha maji machafu katika maeneo wanayoishi.
Haule ametoa wito huo leo katika mkutano wa Baraza la madiwani la kuishia kipindi cha robo ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2024/2025 , uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya kata ya Lyamkena.
Amesema kuwa, ipo haja ya kuchimba mashimo ya taka hasa maeneo ya vijijini ambapo taka zimekuwa nyingi, ili kuepusha kuzagaa kwa taka na katika maeneo ya Mjini takataka zihifadhiwe na kufata utaratibu uliowekwa na Halmashauri ambapo ili kurahisisha ukusanyaji wake.
Awali, mwenyekiti wa kamati ya mipango miji na Mazingira ,Mhe. Navy Sanga akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo amesisitiza suala la tozo ya kiasi cha shilingi Elfu hamsini kwa kosa la uchafuzi wa mazingira na kuwataka wataalam wa mazingira kusimamia sheria za usafi wa mazingira.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa