Na. Lina Sanga
Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Makambako,Mhe. Hanana Mfikwa leo katika Mkutano wa baraza la Madiwani la robo ya nne kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kwa kuwataka wakuu wa taasisi za Serikali na binafsi kushirikiana katika shughuli mbalimbali ili kujenga mahusiano mazuri baina ya taasisi zao.
Mhe. Hanana amesema hayo baada ya kuwasilishwa kwa taarifa ya tuzo ya utendaji bora ya Halmashauri ya Mji Makambako iliyowasilishwa na Mkuu wa Idara ya Utumishi,Norbetha Nyoni na kuwataka wakuu wote wa taasisi kuendelea kushirikiana ili Halmashauri ya Mji Makambako iendelee kuwa bora katika utendaji wa kazi mbalimbali na kupata maendeleo ni lazima kuwe na ushirikiano wa taasisi moja na nyingine,hivyo kila taasisi ijitahidi kushirikiana na taasisi zingine zilizopo katika Halmashauri ya Mji Makambako ili kuijenga Halmashauri,Wilaya ya Njombe na Mkoa kwa ujumla kwa umoja.
"TRA wakishirikiana na taasisi zingine kuhamasisha wananchi kulipa kodi itasaidia kuwafikishia walengwa ujumbe huo kwa wakati na kama Jeshi la Wananchi (JWTZ) wamepata msiba wote kwa pamoja tukajumuika na kushirikiana itazidi kuimarisha kujenga mahusiano mazuri baina yetu",alisema Mhe. Hanana.
Aidha,ameishukuru Serikali na Wizara ya Kilimo kwa kufanya jitihada ya upatikanaji wa mbolea ya ruzuku ili kuwawezesha wakulima kupata mbolea kwa bei nafuu na ameiomba wizara ya Kilimo kuhakikisha mbolea ya ruzuku inawafikia wakulima kwa wakati ili waweze kulima kulingana na msimu na kupata mavuno ya kuridhisha.
Ametoa wito kwa wakulima wote kujisajili kwa wakati uliopangwa ili kupata mbolea ya ruzuku kwa wakati ,pia ametoa wito kwa waheshimiwa madiwano wote kuhamasisha wakulima waliopo kwenye Kata zao ili wapate mbolea kwa wakati.
Akiwasilisha taarifa kuhusu mbolea ya ruzuku,Kaimu Mkuu wa idara ya Kilimo,Bi. Beatrice Tarimo amesema kuwa mbolea ya ruzuku itatolewa kwa wakulima waliosajiliwa pekee,katika Mtaa au Kijiji anacholima ili kupata takwimu sahihi za wakulima na ukubwa wa mashamba yao.
Amesema kuwa usajili wa wakulima utaanza rasmi Agosti 9,mwaka huu katika Mitaa na Vijiji ambavyo shughuli ya kilimo zinafanyika na baada ya usajili wakulima watanunua mbolea ya ruzuku kwa wafanyabiashara wa pembejeo za kilimo waliosajiliwa kuuza mbolea kwa bei elekezi ya mbolea yenye ruzuku kulingana na ukubwa wa shamba analolima.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa