Afisa utamaduni Halmashauri ya Mji wa makambako Esther Mwakalindile Pichani akisoma Risala fupi kwa wageni waalikwa na wadau mbalimbali waliohudhulia katika Tamasaha la Sanaa kwa Shule za Msingi Halmashauri ya Maji wa Makambako ,Tamasha ambalo limefanyika mnamo taarehe 13/11/ 2020 katika Uwanja wa Amani.Katika risala hiyo afisa utamaduni na michezo ameeleza kuwa dhima na lengo ya kufanyika kwa tamasha hilo ni :Kuibua vipaji mbalimbali vya Wanafunzi ambavyo wamepewa na mwenyezi Mungu kwa kujifunza ama kuzaliwa navyo ,Kuwasaidia wanafunzi kuwa na ujasiri wa kutetea ndoto zao hasa kwa kuona Maigizo na Michezo mbalimbali ambayo itaoneshwa na Wanafunzi hao ,kuleta burudani na ushirikiano kwa wanafunzi wote wa Shule za Msingi Halmashauri ya Mji wa Makambako ,Kuwajengea uwezo Wanafunzi hasa kujieleza pindi wanapokutana na changaomoto katika kutimiza ndoto zao za hapo baadae ,kuwakumbusha Walimu kujitoa hasa katika masuala mazima ya kuwasaidia Wanafunzi katika kuibua vipaji vyao na kuwatia moyo Walimu wasikate tamaa ya kuwasidia wanafunzi katika nyanja mbalimbali hususani masuala ya michezo na Sanaa.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa