Wanafunzi kutoka shule mbalimbali za Msingi Halmashauri ya Mji wa Makambako wakiwasikiliza Wanafunzi wenzao kutoka Shule ya Msingi Maendeleo wakati wa kuigiza igizo ambalo limeonesha Makundi mawili ya Wanafunzi ambapo kundi la kwanza ni Wanafunzi ambao wanania na malengo ya kufika mbali na wanafuata kile kimewapeleka shule wakati kundi la pili ni Wanafunzi ambao wapo Shule na wanafuata mambo ambayo yapo nje na Masomo mwisho wa siku kundi ambalo lipo shule na michanganyo wengi wao wameshindwa kutimiza ndoto zao na kuishia mtaani kujilaumu na kujuta wakati tayari muda umesonga na haurudi nyuma ,Waigizaji wamehitimisha kwa ujumbe wa "Majuto ni Mjukuuu "na "Mshika mawili moja huponyoka" ,kwamba Wanafunzi wanatakiwa kuwa makini katika kutimiza ndoto zao kwani kuna vitu vingi kama wasipokuwa makini vinaweza kufifisha ndoto zao za kusonga mbele kitaaluma.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa