Na. Lina Sanga
Arusha
Wizara ya TAMISEMI kupitia Mamlaka za Mikoa na Halmashauri zote ý kutekeleza matumizi ya mifumo ya mtandao kutoa huduma kwa umma pamoja na kuhuisha tovuti zote za taasisi.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu Tawala Mkoa wa Njombe,Bi. Judica Omari mbele ya Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Mhe. Jenista Mhagama katika Kikao kazi cha tatu cha Serikali Mtandao, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa AICC jijini Arusha kwa siku tatu kuanzia Februari 8 hadi februari 10.
Bi. Judica amesema kuwa,kwa sasa Mikoa na Halmashauri zote zitaongeza utoaji huduma kidigitali kwa kutumia mifumo ya Serikali mtandao, ikiwa ni pamoja na kuendesha vikao vyote vya kisheria ili kupunguza gharama za uendeshaji na kuhuisha kwenye mabaraza la madiwani.
Aidha amesema kuwa, Mamlaka za Mikoa na Halmashauri zitasimamia sheria ya Serikali mtandao ya mwaka 2019 ,pamoja na kanuni zake za mwaka 2020 na kuanzisha na kuziendeleza kamati za TEHAMA kwenye taasisi zote lengo ikiwa kuongeza matumizi ya mifumo ya mtandao nchini kutoka asilimia 40 hadi kufikia asilimia 80 mwaka 2025.
Ametoa rai kwa Mamlaka ya Serikali Mtandao kuzishindanisha Mamlaka za Mikoa na Halmashauri katika utekelezaji wa sheria ya Serikali Mtandao,ili kuhakikisha utekelezaji wa sheria hiyo unafanyika kwa asilimia ya juu.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa